De Gea aigomea Man United, PSG yamtolea macho

Muktasari:

  • Kipa huyo amekuwa katika kiwango cha juu na kuisaidia Manchester United katika michezo mingi ya Ligi Kuu

London, England. Manchester United ipo katika presha kubwa ya kuuza kipa wake David de Gea baada ya ‘kukataa dau la mwisho alilopewa’ huku Paris Saint-Germain ikiwa tayari kumsajili kwa pauni 60milioni.

Mabingwa wa Ufaransa, PSG wapo tayari kumlipa De Gea kiasi anachotaka cha pauni 350,000 kwa wiki huku wakiweka wazi wapo tayari kutoa pauni 60milioni kumsajili msimu huu.

De Gea ameshinda tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu England katika misimu mitano kati ya saba, huku ndani ya Man United ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa misimu minne mfululizo kati ya 2014 and 2018.

Vyanzo vya ndani vya mtandao wa The sun, vimebaini kuwa kipa huyo, anadaiwa kuweka wazi kwamba hayupo tayari kuendelea kusalia Old Trafford msimu ujao wa 2019/20.