Dewji awashukia wachezaji wavivu Simba

Friday February 8 2019

 

By Abel Charles

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ametangaza hali ya hatari kwa wachezaji wanaocheza chini ya kiwango ndani ya kikosi cha timu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo, Dewji alisema kuwa bodi ya Simba haiko tayari kuendelea kubaki na wachezaji ambao hawajui thamani ya jezi ya klabu hiyo.

"Tumekubaliana kwamba wale wachezaji wasio na nidhamu na wasiojituma basi wajiandae kuondoka lakini kama wataamua kujitolea na kuvuja jasho lao kwa ajili ya timu tutaendelea nao," alisema Dewji.

Kwenye mechi tatu za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba imepata ushindi wa mechi moja na kupoteza mbili. Ikifunga mabao matatu na kufungwa 10.

 

Advertisement