Dybala aitosa Manchester United kimtindo

Saturday May 25 2019

 

Turin, Italia. Kiungo wa Juventus, Paulo Dybala amesema hana mpango wa kujiunga na Manchester United kwa sasa.

Wakala yake ambaye ni kaka yake, Gustavo amemtaka Dybala kuondoka Juventus kwenda kupata changamoto mpya.

Dybala ni miongoni mwa wachezaji nyota waliopo katika orodha ya kocha Ole Gunna Solskjaer.

Ujio wa mshambuliaji nguli Cristiano Ronaldo unaonekana kumfunika Dybala ambaye amekuwa na kiwango bora kwa Kibibi hicho Kizee cha Turin.

“Hii nafasi yake nzuri ya kuondoka kwenda kupata changamoto mpya,” alisikika akisema Gustavo alipohojiwa na redio nchini Argentina.

Mchezaji huyo alisema licha ya kupewa ushauri na kaka yake, lakini anataka kubaki Juventus.

Advertisement

Advertisement