Fainali za Kombe la Dunia 2026 kuchezwa nchi tatu

Muktasari:

Nchi za Marekani, Canada na Mexico zimepewa hakin ya kuandaa fainali za Kombe la Dunia baada ya mkutano mkuu wa Fifa kuzipigia kura dhidi ya Morocco.

 

Moscow. Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2026 zitarudi tena barani Amerika Kusini baada ya Mkutano Mkuu wa Fifa kuzipa nchi za Marekani, Canada na Mexico haki ya kuandaa michuano hiyo mikubwa ya soka duniani.

Morocco, ambayo iliingia tena kwenye kinyang'anyiro cha kuwania uenyeji wa fainali hizo baada ya kushindwa mara mbili, ilizidiwa nguvu na umoja huo.

Michuano hiyo itarudi Amerika Kaskazini miaka 32 baada ya Marekani kuwa mwenyeji wa fainali hizo mwaka 1994.

Katika kura zilizopigwa leo Jumatano, Marekani, Canada na Mexico, ambazo zitakuwa nchi tatu za kwanza kuandaa fainali hizo kwa pamoja, zilipata kura 134 (sawa na asilimia 67, wakati Morocco ilipata kura 65 sawa na asilimia 33 ya kura zote.

Awali, Morocco iliahidi kuwa iwapo ingepata uenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2026, ingeipa FIFA kiasi cha Dola 5 billioni (sawa na Sh10 trilioni) kama faida itakayopatikana kwenye mashindano hayo.

Muungano wa Marekani, Canada na Mexico umeshinda zabuni ya kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2026 na kuiangusha Morocco, ambayo nayo iliomba nafasi hiyo.

Zoezi la upigaji kura kwa ajili ya kumpata muandaaji wa Kombe la Dunia 2026, litaendeshwa kwa mfumo wa Kielektroniki.

Pia Ushirika wa Marekani, Canada na Mexico awali uliahidi kutoa faida ya Dola 11 bilioni (Sh 22 trilioni) kama faida ambayo FIFA itapata baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia iwapo utapata nafasi ya kuandaa fainali hizo mwaka 2026.