Fifa yamfungia Malinzi miaka 10 kwa matumizi mabaya ya fedha

Muktasari:

Malinzi pia alipokea dola 55,000 fedha ambazo zilikuwa zawadi kwa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania U17 kwa kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika 2017 Gabon.

ZURICH, Uswisi. Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) limemfungia miaka 10, rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi kwa matumizi mabaya ya fedha za shirikisho hilo.

Fifa imesema Malinzi alipokea dola 528,000 ukiwa ni mkopo kwa miaka minne aliyokuwa madarakani, lakini alishindwa kutoa taarifa sahihi ya matumizi ya fedha hizo.”

Malinzi pia alipokea dola 55,000 fedha ambazo zilikuwa zawadi kwa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania U17 kwa kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika 2017 Gabon.

Fifa alisema Malinzi aliyekuwa mjumbe kamati ya maendeleo alikuwa akitoa fedha katika miradi yote duniani wakati alipokuwa katika jukumu hilo kuanzi 2013-17 ndipo alipochukua fedha hizo.

Malinzi pia anatakiwa kulipa faini ya dola 503,000 kwa Fifa.