Guardiola alilia penalti mbili ilizonyimwa Manchester City

Muktasari:

Kocha wa Manchester City ametoa matamshi makali kwa mwamuzi wa mechi ya jana Mike Dean kwa madai ya kuwanyima penalti mbili dhidi ya Liverpool.

London, England. Kocha Pep Guardiola amechukizwa Manchester City kutopewa penalti mbili alizodai zilikuwa halali katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool.

Guardiola alionekana akimtolea maneno makali mwamuzi namba nne wa mchezo Mike Dean kabla ya kushikana mkono na mwamuzi wa kati Michael Oliver.

Kocha huyo alidai Man City ilistahili kupewa penalti mbili katika mchezo huo ambao timu hiyo ilifungwa mabao 3-1, yaliyofugwa na Fabinho, Mo Salah na Sadio Mane.

Matokeo hayo yameifanya Liverpool kufikisha pointi 34 na Man City 26 katika msimamo wa Ligi Kuu na zote zimecheza mechi 12 kila moja.

Guardiola alilalamikia tukio la kwanza la beki Trent Alexander-Arnold kushika mpira akiwa ndani ya eneo la hatari.

Hata hivyo, msaada wa teknolojia ya VAR ilipotumika ilionekana kama kinda huyo hakukusudia kushika mpira.

Alexander-Arnold alishika tena mpira akiwa ndani ya eneo la hatari, lakini Oliver alisema haikuwa penalti.

Matukio yote mawili yalimfanya kocha huyo kutoa kauli kali kwa Dean akidai Man City haikutendewa haki.

Wakati wachezaji wakishikana mikono baada ya mpira kumalizika, Guardiola alimfuata Oliver na kumwambia: ‘Asante. Asante sana’.

Kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich alisema hana namna zaidi ya kuipongeza Liverpool kwa matokeo hayo.

&&&&&&&&&&&

 

Ronaldo achukia kutolewa mapema Juventus ikichapa AC Milan

S. Hii ni mara ya kwanza kwa Ronaldo kutolewa mapema ndani ya mchezo tangu alipojiunga na Juventus akitokea Real Madrid msimu uliopita.

Milan, Italia. Mshambuliaji nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo amechukizwa na uamuzi wa kutolewa mapema wakati timu yake ikishinda bao 1-0 dhidi ya AC Milan kwenye U.

Ronaldo hakufurahishwa na uamuzi wa kocha Maurizio Sarri alipomtoa dakika ya 55 na kuingia Paulo Dybala.

Ronaldo hakushikana mkono na Sarri wakati akieenda kwenye benchi, pia alitoka uwanjani kabla ya mpira kumalizika.

Wakati akitoka nje, mshambuliaji huyo alikuwa amekunja sura akionyesha kuchukizwa na uamuzi huo.

Mabadiliko ya Sarri yalikuwa na maana kwani Dybala alifunga bao hilo dakika ya 77 na kuipa pointi tatu Juventus.

Matokeo hayo yameifanya Juventus kuendelea kukaa kileleni katika msimamo wa ligi mbele ya Inter Milan.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ronaldo kutolewa mapema ndani ya mchezo tangu alipojiunga na Juventus akitokea Real Madrid msimu uliopita.

Taarifa zilisema Sarri alichukua uamuzi huo akihofia Ronaldo kupata maumivu.

Awali, Ronaldo hakuwa na furaha alipotolewa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Lokomotiv Moscow, ingawa Sarri alisema alimtoa baada ya kulalamikia maumivu ya goti.