Guardiola arejea Barcelona

Saturday April 25 2015

Zurich, Uswisi Ni kama kocha Pep Guardiola amerejeshwa Barcelona kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Bayern Munich na Barcelona unaoitwa fainali.

Mchezo huo wa Mei 5, utakuwa kivutio zaidi kwa kocha Guardiola aliyeko Bayern aliyekulia na kucheza soka Barcelona, klabu aliyoiwezesha kucheza nusu fainali mara nne, akifanya hivyo mara mbili akiwa Bayern .

Guardiola, (pichani) Ialiipa taji Barcelona hilo mwaka 2009 na 2011, jambo linalomweka kwenye nafasi ya kuongeza kitu kwenye jina lake, endapo ataivusha Bayern dhidi ya Barcelona.

Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa pia wa kuzikutanisha klabu mbili za Hispania kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikiwa ni mara ya kwanza.

Klabu hizo zinapokutana, pambano baina yao, ‘El Clasico’ hugeuka kivutio kikubwa, si Hispania pekee, bali katika sehemu mbalimbali Ulaya na duniani.

Pia, kitu kingine cha kuvutia ni kwa kocha Carlo Ancelotti wa Real Madrid ambaye naye anakutanishwa na Juventus, mojawapo ya klabu kubwa alizowahi kufundisha.

Advertisement