Jinsi Simba B walivyotua Zanzibar leo

Wednesday January 9 2019

 

By Mwanahiba Richard

Kikosi cha wachezaji saba kutoka timu ya vijana ya Simba kimewasili kisiwani Unguja kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi kilichobaki.

Kocha Patrick Aussems amewacha baadhi ya wachezaji kisiwani hapa ambao watacheza mechi ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi ambayo itachezwa keshokutwa Ijumaa.

Kikosi hicho kimeongozwa na kocha wao Nico kiondo ambaye amesema atafuata programu iliyoachwa na bosi wake Aussems.

"Wachezaji niliokuja nao ni wazuri na wapambanaji, naamini watafanya vizuri kufikia malengo ya klabu ambayo pia ni kutwaa ubingwa wa mashindano haya.

"Hawa wachezaji ni wageni kwenye michuano hii lakini wamecheza mashindano makubwa zaidi ya haya hivyo sina hofu kabisa katika kutimiza malengo," alisema Kiondo.

Advertisement