Kaburu aibuka uwanja kuishuhudia Simba, Prisons

Thursday November 7 2019

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Saa 48, baada ya kuachiwa kwa dhamana Makamu wa rais wa zamani wa Simba, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ ameibukia Uwanja wa Uhuru na kuishuhudia Simba ikicheza mechi yake dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kaburu mmoja wa wapenzi wa kubwa wa soka ikiwa ni siku yake ya tatu akiwa nje baada ya kupata dhamana alionekana jukwaani uwanja wa Uhuru kushuhudia timu yake ya Simba.

Kaburu aliingia uwanjani hapo mpira ukiwa tayari umeanza na kwenda kukaa jukwaa kuu upande ambao mara nyingi hukaa mashabiki wa Simba.

Wakati anakwenda kukaa jukwaani alisalimiana na watu mbalimbali akiwemo mashabiki na mwanachama wa Simba na kuiibua shangwe.

Kaburu na aliyekuwa rais wa Simba, Evans Aveva waliachiwa kwa dhamana baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwaondolea shtaka la utakatishaji wa fedha, lililowafanya kukaa ndani kwa zaidi ya miaka miwili.

Advertisement