Kagera Sugar yaweka silaha zake hadharani tayari Ligi Kuu

Tuesday July 9 2019

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Kikosi cha Kagera Sugar kimeweka wazi kukamilisha usajili wao kwa asilimia 88 na wamebakisha wachezaji watatu kwa nafasi ya kipa, kiungo na mshambuliaji watatoka Uganda.

Katika asilimia hiyo, Kagera Sugar imewataja sehemu ya wachezaji wanaounda timu hiyo kwa sasa ni kipa Said Kipao, Mwaita Gereza, Ally Shomary, Haroun Kheri na David Luhende.

Wengine ni Juma Shemvuni, Juma Nyosso, Erick Kyaruzi, Hassan Isihaka, Majidi Khamis, Zawadi Mauya, Moussa Hadji Mosi, Ally Ramadhani na Abdallah Seseme.

Wengine ni Peter Mwalyanzi, Japheth Makalayi, Yussuf Muhilu, Geofrey Mwashiuya, Awesu Awesu, Chalamanda, Erick Mwaijage, Frank Ikobela, Everist Mujwahuki na Nassor Kapama.

Mabosi wa Kagera Sugar wameweka wazi kuwa nafasi za wachezaji hao watatu watasajiliwa kutoka sehemu mbalimbali. Kiungo anatarajiwa kutoka Zanzibar na mshambuliaji watamtoa Uganda.

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime hakutaka kumtaja mchezaji na kusisitiza ukifika wakati kila kitu kitakuwa wazi.

Advertisement

Advertisement