Kiemba: Wachezaji Taifa Stars waandaliwe kisaikolojia

Saturday May 25 2019

 

By Eliya Solomon

Dar es Salaam. Kiungo wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Amri Kiemba amesema wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania wanatakiwa kuandaliwa kisaikolojia kabla ya fainali za mataifa ya Afrika nchini Misri.

Fainali za Mataifa ya Afrika nchini Misri zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi, Juni 21 hadi Julai 19 mwaka huu  katika miji minne tofauti nchi humo.

Kiembea alisema inawezekana wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia waliofanya maajabu katika fainali za mwaka 2012 siri yao kubwa ni kuandaliwa kisaikolojia.

“Lazima tutambue kuwa mpira unaanzwa kuchezwa kichwani, inatakiwa waandaliwe kisaikolojia alafu tuone namna ambavyo wanaweza kufanya vizuri.

“Wanaweza wasichukue ubingwa, lakini wakaonyesha kiwango ambacho kila mmoja wetu atavutiwa nacho,” alisema kiungo huyo wa zamani wa Simba.

Advertisement