Kiungo Ally Ng’anzi awapagawashia Wazungu Marekani

Saturday May 25 2019

 

By Thomas Ng'itu

Dar es Salaam.Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Ally Ng'anzi anayekipiga kwa mkopo katika klabu ya Minessota inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza nchini Marekani ameendelea kukonga nyoyo za mashabiki wa timu hiyo kutokana na kiwango chake.
Ng'anzi aliyekuwa anaichezea Singida United alisajiliwa na MFK Vyskov inayoshiriki Ligi Daraja la pili nchini Czech.
Baada ya kutua katika timu hiyo, waliamua kumtoa kwa mkopo Minessota ambayo nyota yake imeanza kung'aa baada ya kukubalika na mashabiki wa timu hiyo.
Meneja wa mchezaji huyo, Zuberi Kambi alisema anafurahishwa na namna ambavyo kijana wake amepokelewa nchini humo licha ya kuwa na muda mfupi.
"Inapendeza kuona watu wa eneo husika wakikubali kile ambacho unafanya ni jambo zuri na haya yote yanatokana na mchezaji mwenyewe kujituma na kutambua kitu gani anakitafuta," alisema Kambi.
Aliongeza anataka kuhakikisha anawatafutia wachezaji wake nafasi ya kutoja na kwenda kujaribu kucheza soka la kukipwa nje ya nchi.
Kambi anawasimamia Feisal Salum, Mohammed Issa 'Banka', Hassan Dilunga, Ally Ng'anzi na Charles Masenga.

Advertisement