Klopp ampiga kijembe Guardiola

Muktasari:

  • Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema wataendelea kutumia mfumo wao wa uchezaji bila kuangalia wapinzani wao Manchester City wanacheza staili gani.

London, England. Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amesema Liverpool hawezi kushindana na Manchester City kwa kuwa kila timu inacheza soka kwa staili yake.

Klopp ametoa kauli hiyo baada ya Liverpool kuilza Chelsea mabao 2-1 dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jana jioni.

Alisema hatishiki na ushindi mkubwa wa Man City wa mabao 8-0 iliyopata dhidi ya Watford juzi, Jumamosi. Kauli ya Klopp ni kijembe kwa kocha Pep Guardiola aliyewajibu waliombeza baada ya kuchapwa 3-2 na Norwich City.

Timu zimeanza vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England kama ilivyokuwa msimu uliopita. Liverpool inaongoza kwa pointi 18 na Man City 13.

“Si klabu zote zinazocheza mfumo unaofanana kila moja ina staili yake ya kucheza. Lakini, jambo la msingi ni kucheza kwa kiwango bora na kupata ushindi,”alisema kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund.

Klopp alisema Ligi Kuu ni mashindano ambayo kila timu ina wajibu wa kucheza soka yenye manufaa.

Mabao ya beki wa kulia Trent Alexander-Arnold alilofunga kwa kiki ya mpira wa adhabu na lile la kichwa kupitia kwa Roberto Firmino yalitosha kuongeza pengo la pointi baina ya timu hizo.

Kocha huyo alisema haikuwa kazi rahisi kupata ushindi dhidi ya Chelsea inayoundwa na idadi kubwa ya wachezaji chipukizi wenye kasi.