Kocha Emery: Hadi kieleweke tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

Friday March 15 2019

 

Kocha wa Arsenal amesema atajisikia fahari kushinda taji lake la kwanza akiwa na klabu hiyo baada ya jana timu yake kupindua matokeo ya kichapo cha 3-1 na kufuzu robo fainali ya Europa League kwa jumla ya mabao 4-3.

Arsenal ilifanikiwa kuifunga Rennes ya Ufaransa mabao 3-0 yaliyofungwa na  Pierre-Emerick Aubameyang aliyefunga mawili dakika ya 5 na 72 na lingine likifungwa na  Ainsley Maitland-Niles dakika ya 13.

Emery ambaye amewahi kuchukua ubingwa wa mashindano hayo mara tatu  amesema wanaona uwezekano wa kushinda taji hilo.

Kocha huyo anaona hiyo ni nafasi yao ya kupata tiketi ya ziada kutinga Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao kama watachukua ubingwa wa Europa League kwani kupata nafasi hiyo kwa kutegemea ubingwa wa Ligi Kuu England ni kazi ngumu.

Advertisement