Kocha Madagascar: Hatuwezi kufunika mafanikio ya Afcon 2019

Friday July 12 2019

 

By AFP

Cairo, Misri. Kocha wa Madagascar, Nicolas Dupuis amesema katika fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) itakuwa vigumu kwa nchi hiyo, iliyoshiriki kwa mara ya kwanza mwaka huu, kufunika mafanikio yao ya kufika hadi robo fainali.
Nchi hiyo ambayo ni kisiwa katikia Bahari ya Hindi ilijikuta ikikatisha ndoto yao jana A|lhamisi ilipofungwa mabao 3-0 na Tunisia, ambayo katika orodha ya ubora ya Fifa iko juu kwa nafasi 83.
"Najivunia kile wachezaji walichofanya tangu mwanzoni mwa mashindano. Nawavulia kofia," alisema Dupuis, ambaye mkataba wake ulikuwa unaisha mwishoni mwa mashindano hayo yanayoendelea nchini Misri.
"Leo ngazi zilikuwa juu sana. Lakini kwa kuangalia mbele, si kitu kikubwa. Kipa umbele changu ni Madagascar."
Dupuis alianza kufundisha timu hiyo mwaka 2017 na amefanikiwa kuibadilisha nchi hiyo ambayo wakati fulani iliwahi kushika nafasi ya 190 kwa ubora duniani na ambayo ililkazimika kupitia michuanbom ya awali kabla ya kufika fainali hizo na kushangaza wengi.
"Sijui kama kipa umbele cha Madagascar ni kuendelea kuwa nami," alisema Dupuis.
"Itakuwa vigumu kufanya vizuri ziidi (ya mwaka huu). Kuna kazi kubwa ya kufanya nchini Madagascar. Hatuna budi kutumia kile tulichofanya kuonyesha kuwa kujitahidi hulipa.
"Tunahitaji kuendelea kufanya kazi la sivyo itakuwa kitu cha muda. Tunahitaji kurudi kazini. Sijutii. Tulikumbana na timu nzuri sana."

Advertisement