Kocha Serengeti Boys aigeukia Nigeria

Muktasari:

  • Mirambo alisema kitendo cha Serengeti Boys kucheza na timu za Ulaya katika mashindano ya Uefa Assist kimewaweka katika mazingia mazuri wachezaji wake. Serengeti Boys inajifua Uwanja wa JK Youth Park, Dar es Salaam huku ikijiandaa kwenda Dubai.

Dar es Salaam. Kocha wa Serengeti Boys Oscar Mirambo amesema hatishwi na ubora wa wapinzani waliopangwa kundi moja katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana (Afcon U17).

Serengeti Boys imepangwa Kundi A na Angola, Nigeria, Uganda. Kundi B linaundwa na Cameroon, Senegal, Morocco na Guinea.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mirambo alisema amepata bahati ya kuwasoma wapinzani wao walipokuwa Uturuki kwenye mashindano ya Uefa Assist.

Mirambo alisema hakuna timu isiyofungika katika fainali hizo kwa kuwa ameziona kupitia mashindano ya Uefa Assist.

“Soka wanalocheza wapinzani wetu halina tofauti sana na kwetu, karibu timu zote zitakazocheza Afcon tulikuwa nazo Uturuki tumezisoma na wachezaji wangu wamejiandaa vizuri kuzikabili,” alisema Mirambo.

Mirambo alisema kitendo cha Serengeti Boys kucheza na timu za Ulaya katika mashindano ya Uefa Assist kimewaweka katika mazingia mazuri wachezaji wake. Serengeti Boys inajifua Uwanja wa JK Youth Park, Dar es Salaam huku ikijiandaa kwenda Dubai.

Timu zitakazofuzu robo fainali katika fainali hizo zitakazoanza Aprili 14 hadi 29, Dar es Salaam zitacheza kombe la dunia kwa vijana.