Kumbe mabao ya Okwi Simba yanatoka hapa!

Wednesday January 16 2019

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam.  Kama ulikuwa hujui siri ya mabao ya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi raia wa Uganda, sasa mwenyewe amefafanua kila kitu.

Okwi ambaye tangu ajiunge na Simba katika vipindi tofauti,  amekuwa anafanya vizuri.

MCL Digital imemshuhudia akifanya maombi kabla ya kuingia uwanjani kufanya mazoezi na alipoulizwa alisema.

"Hii ni kawaida yangu,  kila ninapoingia kufanya mazoezi lazima nianze kwa maombi na tunapomaliza huwa nafanya yale ya pamoja,"alisema Okwi ambaye hata anapoanza kucheza mechi,  huwa anafanya maombi.

Kitendo ambacho Okwi amekifanya hutokea kwa wachezaji wachache, kila mmoja huwa na staili yake, wengine kutanguliza  aina ya miguu kulia au kushoto.

Advertisement