Lechantre atinga mzula, arudi kwao Ufaransa

Wednesday June 13 2018

 

By THOBIAS SEBASTIAN

KOCHA wa Simba, Pierre Lechantre tayari ameshamalizana na uongozi wa timu hiyo na ameshaondoka hapa nchini alfajiri ya leo Jumatano.

Lechantre baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa Simba jana Jumanne alichukua kila kilichochokuwa chake na alianza safari ya kwenda kwao Ufaransa.

Mfaransa huyo aliyeisaidia Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya Wekundu hao wa Msimbazi kushindwa kufanya hivyo kwa miaka mitano. Alimaliza mkataba wake wa miezi sita wa kukinoa kikosi hicho na uongozi kushindwa kuingia makubaliano ya kumuongezea mkataba mpya.

"Kuna mambo muhimu ambayo tulishindwa kufikia makubaliano katika mkataba mpya basi nikashindwa kuongeza mkataba niwashukuru viongozi, wachezaji, wanachama na wapenzi wa Simba kwa muda wote niliokuwa nikifanya kazi hapa nchini," alisema Lechantre.

Advertisement