Lukaku sasa aiweka mtegoni Man United

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo amerejea katika kiwango chake baada ya kuivusha Man United katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Brussels, Ubelgiji. Mshambuliaji nyota Romelu Lukaku ameiweka njia panda Manchester United baada ya kukumbwa na majeruhi.

Lukaku anatarajiwa kufanyiwa kipimo cha MRI katika mguu baada ya kupata maumivu.

Taarifa za ugonjwa wake zimekuja wakati nyota huyo akiwa kambini na kikosi cha Ubelgiji kinachojiandaa na mechi za kimataifa wiki hii.

Lukaku juzi hakufanya mazoezi na alitarajiwa kupimwa kujua ukubwa wa jeraha lake.

Mshambuliaji huyo amerejea katika kiwango chake baada ya kuivusha Man United katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Taarifa hizo zinaweza kumshitua kocha wa Man United Ole Gunnar Solskajer ambaye anajiandaa kwa mechi kali ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona siku chache zijazo.