MO Dewji ambakisha Mkude Simba

Friday May 24 2019

 

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Simba Mohamed Dewji 'MO' amethibitisha kwamba kiungo na nahodha wao wa zamani Jonas Mkude hataondoka klabuni hapo.

MO kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram amewashusha presha mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuwa kiungo huyo ataendelea kuwepo.

MO ametuma ujumbe huo ulioambatana na picha akiwa na Mkude wakiwa wanapeana mikono

Taarifa hiyo inazima uvumi kuwa Mkude anakaribia kuondoka klabuni hapo huku baadhi ya vyombo vya habari (sio kutoka kampuni ya Mwananchi Communications) vikidai kiungo huyo anakaribia kutua Yanga.

Licha ya Simba kutamka kwamba itafanya usajili wa nguvu lakini mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo bado hawajaweka wazi wachezaji watakaowaacha.

Advertisement