VIDEO: Mabarafu yawapeleka puta nyota Stars

Muktasari:

  • Kilimanjaro Stars inashika nafasi ya pili katika kundi B ikiwa na pointi tatu, nyuma ya Kenya inayoongoza baada ya kukusanya pointi sita.

Kampala. Mbinu ya benchi la ufundi la timu ya taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' kutumia barafu ili kupooza miili ya wachezaji imeonekana kuwa mwiba kwa nyota wa kikosi hicho.
Wachezaji  wa  Kilimanjaro Stars wamekuwa wakipata wakati mgumu kuingia katika pipa la plastiki ambalo lina maji yenye barafu na wamekuwa waoga kufanya hivyo.
Utaratibu huo ambao ulianza mara baada ya mazoezi ya jana Jumatano, umekuwa ukifanyika kila wachezaji wanapomaliza programu za mazoezi.
Kundi kubwa la wachezaji limekuwa likionyesha woga wa kuingiza miguu katika maji hayo na kisha kuketi kwa dakika mbili kama ambavyo wanaelekezwa na kusimamiwa na benchi la ufundi
Mazoezi hayo ni maalum kwa ajili ya kujenga ustahimilivu pamoja na kuweka sawa misuli kama alivyoainisha kocha msaidizi Zubery Katwila.
"Haya mazoezi ni kwa faida yenu nyie wachezaji kwani yanasaidia kuweka miili yenu sawa sasa hampaswi kuogopa kuingia humo," alisisitiza Katwila.