Mabosi Yanga wamtuliza Dante, Zahera atoa neno

Tuesday September 10 2019

 

By Saddam Sadick, Mwananchi [email protected]

Mwanza. Mbele ya kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera hakuna kinachoharibika. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya timu hiyo kuvutana kwa muda mrefu na beki wake, Vicent Andrew 'Dante', sasa mambo shwari muda wowote ataonekana uwanjani.

Dante amekuwa katika mvutano na mabosi wake akisisitiza kulipwa malimbikizo ya stahiki zake jambo lililomfanya ashindwe kuungana na kikosi cha timu hiyo iliyoweka kambi mjini Mwanza kujiandaa na pambano la Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Zesco.

Akizungumza leo Jumanne Septemba 10, 2019 Zahera amesema mawasiliano baina yake na Dante ni mazuri, kwamba beki huyo pia anawasiliana vyema na mabosi wa timu hiyo.

Amesema kutokana na mazungumzo hayo kwenda vizuri, Dante anaweza kuungana na wenzake kwenye kikosi kuanzia siku yoyote, kuwataka mashabiki kutulia.

"Hata leo nimezungumza naye akanitumia meseji tatu au niwaonyeshe?” amehoji Zahera

Advertisement