Makamba ajitosa kuichangia Yanga

Muktasari:

  • Yanga inaongoza msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 74 katika michezo 32 iliyocheza huku kocha mkuu, Mwinyi Zahera akisisitiza kutaka ubingwa msimu huu licha ya kupewa presha na Simba yenye pointi 66 katika michezo 25 iliyocheza

Dar es Salaam. Licha ya kuwa shabiki kindakindaki wa Simba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba amesema timu hiyo haipaswi kuwabeza wapinzani wao Yanga katika kipindi wanachopitia sasa.

Yanga inakabiliwa na mtikisiko wa uchumi uliopelekea klabu hiyo kutumia utaratibu wa kuwashirikisha wanachama na mashabiki wao kuwachangia.

"Sio vibaya klabu kutafuta msaada kwa wanachama na ndicho inakifanya Yanga, ingawa Simba hatupaswi kuwabeza kwa kipindi wanachopitia," amesema Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli.

Amesema yeye licha ya kuwa shabiki na mwanachama wa Simba, lakini haoni tabu kuwachangia watani zao Yanga.

"Nitachanga si chini ya Sh 1 milioni, hakuna Simba imara bila Yanga imara," amesema Makamba Leo Aprili 24 alipotembelea makao makuu ya Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tabata Relini jijini Dar es Salaam.

 

Amesema Yanga licha ya changamoto wanazopitia, lakini inafanya vizuri na matokeo yanaonekana kwani timu inapambana.

 

 

S:Endapo Serengeti Boys wangeshinda mechi mbili za makundi wangefuzu kuliwakilishwa bara la Afrika kwenye mashindano ya dunia ambayo Afrika inawakilishwa na timu nne zilizozotinga nusu fainali kwenye Afcon.

Waziri Makamba:Serengeti Boys walipewa presha iliyowazidi umri

Imani Makongoro, Mwananchi

Dar es Salaam.Siku chache baada ya Serengeti Boys kuondoshwa kwenye hatua ya makundi katika fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana (Afcon U17), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Yusuph Makamba amesema timu hiyo ilipewa presha ya mashindano kulinganisha na umri wao.

Serengeti Boys ilifungwa mechi zake zote za Makundi dhidi ya Nigeria, Uganda na Angola katika fainali hizo zinazoendelea jijini Dar es Salaam na kukatisha ndoto ya kucheza kombe la dunia kwa vijana baadae mwaka huu Brazil.

"Bado tuna safari ndefu katika soka, tukumbuke tu hamasa ni hatua ya mwisho kwa mchezaji," alisema Waziri Makamba.

Alisema hata timu ya vijana ya Serengeti haikupaswa kupewa hamasa kubwa kama ambayo ilionekana wakati wa mashindano.

"Tuliwapa presha kubwa kulinganisha na umri wao, tuliwaaminisha kuwa Taifa wamelibeba wao, kitu ambacho kwa vijana wa umri wao hawakupaswa kupewa presha hiyo.

"Ambacho kingefanyika wangeambiwa tu kwamba wakacheze kama ambavyo wamekuwa wakicheza, lakini presha waliyopewa kwa ajili ya mafanikio kwenye mashindano ya Afcon iliwazidi umri," alisema.