Makambo achomoka Yanga, asajiliwa kimyakimya Guinea

Thursday May 16 2019

 

Straika tegemeo wa Yanga, Heritier Makambo, sasa ni rasmi ameshatua Horoya FC ya Guinea.

Taarifa kutoka Guinea zilizothibitishwa na Makambo mwenyewe, zimefichua kuwa Mkongo huyo ametua timu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mwanaspoti lilifichua juu ya Makambo kuikacha Yanga Ijumaa iliyopita iliyokuwa na kichwa cha habari, Makambo atengewa Sh 228 Milioni  na ilithibitishwa ametua rasmi.

Usajili wa Makambo zimekuja katika kipindi ambacho Horoya FC ipo katika vita ya kumbakisha straika wake matata Ocansey Mandela anayetakiwa na Wydad Casablanca.

Makambo alithibitisha taarifa hizo, huku ikielezwa kuwa straika huyo aliyesajiliwa na Yanga msimu huu na kuifungia mabao 20, 16 yakiwa ya Ligi Kuu na Manne ya Kombe la FA, akiambatana na Kocha Mwinyi Zahera.

Naye kipa Klaus Kindoki anayeishi chumba kimoja na Makambo alithibitsiah juu ya Mkongoman mwenzake kusajiliwa rasmi na Horoya iliyocheza makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Advertisement

Horoya nndio timu ya Guinea ambayo imekuwa na mafanikio makubwa kwenye mashindano ya kimataifa na kwa kulidhihirisha hilo, msimu huu ilitinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikotolewa na Wydad Casablanca kwa kipigo cha jumla cha mabao 5-0.

Advertisement