Man United, Arsenal zaonyeshana ubabe! Chelsea hoi

Muktasari:

Manchester United imeendelea kubaki kwenye nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu England huku wakiwa na tofauti ya alama 18 na vinara Manchester City waliojikusanyia pointi 41.

England. Kocha Jose Mourinho amewalaumu wachezaji wake kwa kupoteza nafasi nyingi za kufunga jambo ambalo limesababisha timu hiyo kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Arsenal jana Jumatano usiku.

Matokeo hayo yameiweka Manchester United kwenye ushindani kuwapo kwenye timu nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu England.

Makosa ya David de Gea na Marcos Rojo  yaliigharimu timu yao jambo ambalo limemfanya Mourinho kuwatupia lawama wachezaji wake.

Licha ya Manchester United kupewa sapoti na mashabiki kwenye uwanja wake wa nyumbani, Arsenal ndio walianza kuzifumania nyavu za wapinzani wao kupitia kwa Shkodran Mustafi (26’) huku Anthony Martial akiisawazishia United (30’).

Alexandre Lacazette aliwainua mashabiki dakika ya 68’ huku bao hilo likidumu kwa dakika moja tu ambapo Jesse Lingard aliisawazishia Manchester United mnamo dakika ya 69’.

Matokeo mengine kwa mechi zilizopigwa jana usiku

Burnley 1-3 Liverpool

Everton 1-1 Newcastle United

Fulham 1-1 Leicester City

Wolverhampton Wanderers 2-1 Chelsea FC

Tottenham Hotspur 3-1 Southampton