Man United wapewa Barcelona robo fainali Uefa

Friday March 15 2019

 

Droo ya robo fainali ya Klabu Bingwa Bara la Ulaya (UEFA Champion League) imefanyika leo Ijumaa Nyon, Uswisi ambapo mechi kali ikitajwa kuwa kati ya Barcelona na Manchester United.

Manguli hao wa soka barani Ulaya watacheza mchezo wa kwanza katika Uwanja wa Old Trafford, England na Manchester United atakuwa mwenyeji.

Mechi nyingine Liverpool atawakaribisha FC Porto kwenye Uwanja wa Anfield, Ajax itakuwa nyumbani kukipiga na Juventus wakati Tottenham Hotspour watakuwa wenyeji wa Manchester City na mechi

hizo zitachezwa nyumbani na ugenini.

Katika michuano hiyo, Real Madrid ambao ndio mabingwa watetezi, waliyaaga mapema mashindano hayo.

Madrid chini ya Kocha Zinedine Zidane imechukua mara tatu mfululizo na alipoondoka tu, ikaanza kutetereka kwa kupata matokeo mabaya.

Siku tatu zilizopita, Real Madrid imemrudisha nyumbani Zinedine kuendelea na majukumu yake.

Advertisement