Man Utd, Tottenham zagombea saini ya Straika Matata

Muktasari:

Mshambuliaji huyu mwenye magoli 10 katika mechi 14 amekuwa akimvutia kocha wa Tottenham inayofundishwa na Jose Mourinho.

Kkabu za Manchester Utd na Tottenham Hotspour zimeingia vitani kuwania saini ya mshambuliaji Fenerbahce ya Uturuki,Vedat Muriqi.
Mshambuliaji huyu mwenye mabao 10 katika mechi 14 amekuwa akimvutia kocha wa Tottenham   Jose Mourinho.
Kupitia katika gazeti la Per Milliyet la Uturuki  lilieleza kwamba mchezaji huyo mwenye miaka 25 amekuwa akitafutwa mara kwa mara na Spurs.
Ukali wake wa kutupia wavuni sio tu kwenye klabu yake bali hadi kwenye timu yake ya Taifa Albania kwani  ameweza kufunga magoli 23 mojawapo ni bao alilofunga katika mchezo wao wa hivi  karibuni dhidi ya Uingereza  ambao waichapwa mabao 5-3.
Muriqi pia anawindwa na klabu ya Bournemouth na kinacosubiriwa ni klabu yake kuonyesha wapi anaweza kwenda.