Manchester City yampa Sterling mkataba kufuru

Muktasari:

Sterling amefunga mabao 14, katika mashindano yote msimu huu na amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu.

London, England. Raheem Sterling anatarajiwa kutia saini mkataba na Manchester City utakaomfanya kuwa mchezaji ghali raia wa Uingereza.

Sterling alitia saini mkataba unaomlipa mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki Novemba, mwaka jana.

Kocha wa Man City, Pep Guardiola amevutiwa na kiwango cha Sterling ambaye amekuwa chachu ya mafanikio Etihad.

Mshambuliaji huyo wa England amefunga mabao 14 katika mechi za mashindano mbalimbali msimu huu.

Man City inataka kumuongeza mkataba mpya unaoweza kumpa mshahara wa zaidi ya Pauni 300,000 kwa wiki.

Mkataba wa Sterling unamalizika mwaka 2023, lakini Man City inataka kumuongeza baada ya kupandisha kiwango chake katika Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Sterling yuko sawa mshahara wa kipa wa Manchester United, David de Gea anayelipwa mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki.

Man City inataka kumpiga kitanzi mshambuliaji huyo baada ya klabu za Hispania Real Madrid na Barcelona kutaka saini yake.