Manchester Derby kuna mtu anapasuka

Friday December 6 2019

 

By THOMAS NG'ITU

ACHANA NA kichapo cha Arsenal kutoka kwa Brighton usiku wa jana, unaambiwa kesho Jumamosi kuna kazi katika jiji la Manchester wakati wababe Man City na Man United zitakapopapatuana kwenye Uwanja wa Etihad uliopo katika jiji la Manchester.
Timu hizo zinakutana kila moja ikitoka kupata ushindi, Man City wakiifumua Burnley kwa mabao 4-1 ugenini, wakati Manc United wakiwa Old Trafford wakimtibulia rekodi, Jose Mourinho anayeinoa kwa sasa Spurs kwa kuwafunga mabao 2-1. Mourinho ambaye alitemeshwa kazi Man United miezi kadhaa iliyopita tangu alipotua Spurs alikuwa hajaonja kipigo kwani alishinda mechi mbili za Ligi Kuu na moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakifuzu hatua ya pili kabla ya kufungwa na Mashetani hao.
Mchezo huo wa Etihad unatarajiwa kuwa mkali kutokana na utani  wa jadi uliopo kati ya timu hizi ambazo zinatokea katika jiji moja nchini England.
Lakini pia unaweza kuwa kipimo kuzuri kwa Olle Gunner kama gari lake limeshawaka baada ya ushindi wa The Coys ama walibahatisha, kwa kutakiwa kupata ushindi dhidi ya wenyeji wao ambao watataka ushindi ili kuwafukuzia vinara Liverpool ambao msimu wamekuwa moto.
Man City ndio watetezi na maana hiyo kama itayumba mbele ya Man City watazidi kuongeza pengo la pointi baina yao na Liverpool ambao nao kesho watakuwa na kibarua ugenini dhidi ya AFC Bournemouth.
Mchezo huo ni muhimu zaidi kwa Pep Guardiola ambaye chama lake linashika nafasi ya tatu kwani kama wakishinda wanakuwa na pointi 35 na kuwashusha Leicester City ambao wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 35.
Kwa upande wa mechi nyingine Everton watapambana na Chelsea, Bournemouth vs Liverpool, Tottenham vs Burney Fc, Watford vs Crystal Palace na Aston Villa vs Leicester City.

Advertisement