Manyika naye awatungia wimbo Serengeti Boys

Muktasari:

  • Serengeti Boys imepangwa Kundi A katika mashindano hayo pamoja na Uganda, Nigeria na Guinea. Itafungua dimba dhidi ya mabingwa mara mbili wa michuano hiyo, Nigeria

KOCHA wa makipa wa kikosi cha timu ya taifa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Manyika Peter ametunga wimbo maalumu kwa ajili ya kikosi hicho ambacho kitaiwakilisha Tanzania kwenye fainali za Afrika (AFCON) zinazotarajiwa kuanza Aprili jijini Dar es Salaam.

Manyika alisema, sababu ya kutunga wimbo huo ni kuwaunga mkono vijana hao baada ya kuitoa kimasomaso Tanzania katika mashindano hayo. “Lengo ni kuwaunga mkono Serengeti lakini pia kuwafanya watu watambue umuhimu wa kikosi hicho ambacho ni wawakilishi wa Tanzania. Wadau pia wajitokeze kwa wingi kwa sababu shabiki ni mchezaji wa 12 katika kutafuta ushindi,” alisema.

Amesema, hizo ni amsha amsha watu watambue mashindano yamefika barabarani kwani Aprili si mbali.

Serengeti Boys imepangwa Kundi A katika mashindano hayo pamoja na Uganda, Nigeria na Guinea. Itafungua dimba dhidi ya mabingwa mara mbili wa michuano hiyo, Nigeria