Maproo saba waongeza mzuka Stars, Samatta bado

Tuesday March 19 2019

 

By Eliya Solomon

KIKOSI cha timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterans wakijiaandaa na mchezo dhidi ya Uganda.

Katika mazoezi hayo nyota wanaocheza soka la kulipwa nje ya Tanzania, Himid Mao (Petrojet), Shiza Kichuya (Enppi), Simon Msuva (Al Jadida), Yayha Zaid (Ismailia), Thomas Ulimwengu (Js Saoura), Rashid Mandawa (BDF) na Hassan Kessy (Nkana).

Wachezaji hao walionekana kuwa na morali muda wote ambao walikuwa mazoezini huku wanapopata muda wa kupumzika walikuwa wakitaniana na wenzao.

Katika mazoezi hayo Amunike alikuwa akiwataka wachezaji wake wawe na uharaka katika kufanya maamuzi pindi wanapofika golini.

Wachezaji Mbwana Samatta (Genk), Shaban Chilunda na Farid Mussa (Teneriffe) wao watawasili nchini muda wowote kuanzia sasa kujiunga na wenzao.

Advertisement