Mashabiki Man United wajilipua, bora timu yao Ifungwe kuwakomoa Liverpool

Wednesday April 24 2019

 

Mashabiki wa Manchester United wamejilipua kwa kusema kwamba ni bora timu yao  ifungwe leo na watani zao Man City kuliko ubingwa kwenda kwa Liverpool.

Manchester United inashuka kwenye dimba la Old Traford ikiwa nafasi ya 6 na alama 64. Iwapo timu hiyo itashinda mchezo wa leo itafikisha pointi 67 na kuwa sawa na Chelsea.

Hata hivyo, iwapo itapoteza mchezo huo itakuwa imewapa nafasi Manchester City kufikisha alama 89 ambazo zitawafanya kukalia kiti kileleni.

Katika jambo lisilotarajiwa hizo ndio dua za mashabiki wa Manchester United ambapo wanatamani timu yao ifungwa ili kuipotezea mwelekeo Liverpool ambayo kwa sasa ipo kileleni ikiwa na alama 88.

Chelsea wapo nafasi ya nne wakiwa wamejikusanyia alama 67 huku nafasi ya tatu ikiwa imeshikiliwa na Tottenham wenye alama 70.

Advertisement