Mashindano ya kuhamasisha Uchaguzi Salama na Amani kutimua vumbi Zanzibar

Muktasari:


Ibrahim amesema mshindi wa Ligi hiyo kombe, fedha taslimu Sh5 milioni, kupata nafasi ya kufanya utalii sehemu mbalimbali visiwani humo na ng’ombe mmoja.

Dar es Salaam. Mashindano ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) itaanza kutimua vumbi leo Februari 27, 2020 huku timu 53 zimethibitisha kushiriki katika viwanja mbalimbali visiwani humo.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambapo kati ya timu hizo 53, 45 za Unguja na 8 za Pemba.

Akizungumza na Mwanaspoti Mwenyekiti wa Kamati, Sadiq Ally Hamadi maarufu Flash amesema timu Pemba zitachuana ili kutoa timu mbili ambazo zitakuja kuungana na 30 za Unguja ambazo zitapatikana baada ya makundi.

Ligi hiyo inafanyika kwa awamu ya pili safari hii imebeba kauli mbiu ya ‘Uchaguzi salama na amani’ ikiwa ni kuhamasisha Amani katika uchaguzi mkuu unaofanyika Oktoba mwaka huu.

Mdhamini wa Ligi hiyo, Mohamed Ibrahim maarufu Raza Lee baada ya kugawa vifaa vitakavyotumika kwa wachezaji na waamuzi amesema lengo la kufanya hivyo ni kuwapa fursa vijana kuonyesha uwezo wao.

“Michezo inaleta mshikamano, umoja na amani. Na pia ni njia mojawapo ya kujitengenezea ajira na uhakika kwa kuwa michezo inakuwa Tanzania” amesema Ibrahim

Ibrahim amesema mshindi wa Ligi hiyo kombe, fedha taslimu Sh5 milioni, kupata nafasi ya kufanya utalii sehemu mbalimbali visiwani humo na ng’ombe mmoja.

Hamadi amesema zawadi ya mfungaji bora atapata pikipiki.