Mastaa Yanga waipotezea Lipuli FC

Wednesday March 13 2019

 

By OLIPA ASSA

NYOTA wa Yanga, Deus Kaseke na Andrew Vicent 'Dante' wameizungumzia mechi yao na Lipuli, itakayopigwa Jumamosi ya wiki hii kwamba dakika 90 ndizo zitaamua nani mbabe.

Kaseke anasema hajaona maajabu yoyote kwenye mechi hiyo na kudai anaichukuliwa kawaida kama nyingine ambazo wamezicheza.

"Kitu kimoja ambacho mashabiki hawakijui, ukichukulia mechi kwa papara inakuwa ngumu kufanya vizuri, ndio maana nasisitiza nachukulia kawaida.

"Kikubwa ni mchezaji kutambua majukumu yake kuyafanya kikamilifu kwamba Yanga inahitaji nini kwake katika msimu huu, tunachoambiwa na kocha ni kushinda mechi zote,"anasema.

Kwa upande wa Dante pamoja na kwamba hatacheza mechi hiyo kutokana na kusumbuliwa na enka anadai Yanga ipo kamili na wanahitaji ubingwa.

"Yanga malengo yetu ni ubingwa hizo habari za Dante hachezi au Abdallah Shaibu 'Ninja' kocha ana mbinu kali ambazo naamini zitatupa pointi tatu dhidi ya Lipuli," anasema.

Advertisement