Maugo aula, ampa onyo Twaha

Muktasari:

  • Akizungumza na gazeti hili jana, Maugo alisema udhamini wa PAEG umekuja wakati mwafaka na kusisitiza kuwa umemuongezea chachu ya kupambana na kufanya vizuri ndani na nje ya nchi.

Dar es Salaam. Bondia Mada Maugo ameingia mkataba mnono na Kampuni ya Pan African Entertainment Group (PAEG) ambayo atakuwa balozi wake.

Bondia huyo ambaye anajiandaa kuzichapa na Twaha Kiduku hivi karibuni, anakuwa bondia wa pili nchini kupata mkataba mnono baada ya Hassan Mwakinyo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Maugo alisema udhamini wa PAEG umekuja wakati mwafaka na kusisitiza kuwa umemuongezea chachu ya kupambana na kufanya vizuri ndani na nje ya nchi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa PAEG, Barney Barrow alisema wameamua kumdhamini Maugo kutokana na uwezo wake kwenye ngumi.