Mbappe adai akili yote Afcon

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Mbappe alisema jambo kubwa analowaza kwa sasa ni kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri kwenye mashindano ya Afcon ya vijana yatakayofanyika nchini mwezi ujao.

WACHEZAJI wengi wanaofanya vizuri katika vikosi vya timu za vijana wakiwamo wa umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, wamekuwa wakichukuliwa na klabu za Ligi Kuu.

Lakini kwa upande wa mshambuliaji, Kelvin John ‘Mbappe’, kwake imekuwa tofauti baada ya kusema akili yake haiwazi kukipiga popote hivi sasa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mbappe alisema jambo kubwa analowaza kwa sasa ni kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri kwenye mashindano ya Afcon ya vijana yatakayofanyika nchini mwezi ujao.

“Bado nafikiria kuhusu timu ya Taifa tu, kuhakikisha tunafanya vizuri.”