Dakika 90 kuamua vita ya Mbeya City vs Prisons

Sunday January 14 2018

 

Dar es Salaam. Kikosi cha Mbeya City kinashuka dimbani leo Jumapili kwa lengo la kuweka heshima yake mbele ya maafande wa Tanzania Prisons, mechi inayotarajiwa kupigwa saa kumi jioni kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Awali, kocha wa Mbeya City, Ramadhan Nsanzurwimo alisema mipango yake ni kushinda mchezo huo kwani wanataka kugeuza behewa kwa kuifunga Prisons ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye Ligi Kuu na kuishindani.

Timu hizo za mkoa mmoja leo zinakutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu huku kila upande ukitamba kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo mkali unaotarajiwa kuwa na ushidani mkali.

Kocha huyo Mmalawi  wa Mbeya City atakuwa na kibarua kigumu kutokana na kuwa mechi yake ya kwanza mbele ya watani hao kutoka mkoa huo.

Advertisement