Mchezaji ashtakiwa kwa kumbaka kocha wake Marekani

Wednesday September 11 2019

 

By AFP

Mchezaji wa klabu ya mpira wa miguu wa aina ya Kimarekani ya New England Patriots, Antonio Brown ameingia kwenye utata mpya jana Jumanne baada ya kutuhumiwa kumbaka kocha wake wa zamani na kufunguliwa mashtaka Florida.
Brown, ambaye Jumamosi alisajiliwa na mabingwa hao wa Super Bowl baada ya kuruhusiwa na Oakland Raiders on Saturday, anatuhumiwa kumbaka mwalimu wake wa zamani mwenye umri wa miaka 28, Britney Taylor katika matukio matatu tofauti yaliyotokea mwaka 2017 na 2018.
"Nikiwa muathirika wa ubakaji uiliofanywa na Antonio Brown, uamuzi wa kuzungumza hadharani umekuwa ni mgumu sana," alisema Taylor katika taarifa aliyoitoa kwa kutumia mawakili wake.
"Nimepata nguvu katika imani yangu, familia yangu, na ushuhuda wa watu wengine waliopitia mashambulizi ya kingono. Kuzungumza kunaondoa aibu ambayo nimekuwa nayo kwa mwaka mzima uliopita na kuihamishia kwa mtu anayehusika na kubakwa kwangu."
Baadaye Brown alikana kuhusika na kitendo chochote kibaya, kwa mujibu wa barua yake aliyoipityishia kwa wanasheria wake, akidai kuwa uhusiano wa kimapenzi baina ya wawili hao umekuwa ni wa hiari.
"Brown anakanusha tuhuma zote zilizotolewa na mtuhumu," inasema taarifa hiyo. "Uhusiano wowote wa kimapenzi na Brown ulikuwa wa hiari."
Klabu yake ya Patriots ilitoa taarifa jana Jumanne usiku ikisema imeshataarifiwa na ligi ya mpira wa miguu kuhusu suala hilo.
"Tunajua kuwepo kwa kesi ya madai ambayo iliwasilishwa mapema leo dhidi ya Antonio Brown, pamoja na majibu ya wawakilishi wa Antonio.
"Tunachukuua tuhuma hizi kwa uzito. Kwa mnazingira yoyote yake klabu hii hairuhusu shambulio la kingono.
"Ligi ilitutaarifu kuwa itachunguza. Hatutoa taarifa zaidi wakati uchunguzi huu ukiendelea."
Katika mashtaka hayo, Taylor anadai kuwa alikutana kwa mara ya kwanza na Brown mwaka 2010 alipohudhuria darasa la masomo ya Biblia katika chuo cha Central Michigan.
Baadaye nyoita huyo wa ligi ya mpira wa miguu akamuajiri Taylor mwaka 2017, akisema anamtaka msichana huyo amsaidie kuboresha unyumbufu wake.
Hata hivyo, Brown alimbaka mara mbili wakati wa mazoezi mwaka 2017. Baadaye alimtumia ujumbe ambao umejumuishwa katika kesi hiyo.
Taylor alivunja mkataba baada ya matukio hayo, lakini alimrudia baada ya mchezaji huyo kuomba radhi.
Mei 20, 2018, Brown alimlaza Taylor kwa nguvu na baadaye kumbaka.
"Alijaribu kukataa," akipiga kelele akisema "sitaki" na "acha", lakini Brown aliendelea na kumuingilia kimwili.

Advertisement