Messi agonga mwamba Barcelona

Muktasari:

  • Barcelona imeshindwa kupata ushindi licha ya kuwatumia nyota watatu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Lyon jana usiku.

Paris, Ufaransa. Barcelona imekwaa kisiki mbele ya Lyon licha ya kupiga mashuti 25 langoni mwa wapinzani wao.

Barcelona ikiwa ugenini ililazimishwa suluhu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mjini Paris juzi usiku.

Licha ya safu yake ya ushambuliaji kuundwa na nyota watatu Lionel Messi, Phillipe Coutinho na Luis Suarez ambao mashuti yao yalitua mikononi mwa kipa Marc-Andre ter Stegen.

Pia katika mchezo huo, beki nguli Gerard Pique alifikisha idadi ya mechi 100 za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Wachezaji wengine saba waliocheza mechi 100 Barcelona ni Xavi Hernandez, Lionel Messi, Andres Iniesta, Carles Puyol, Victor Valdes na Sergio Busquets.

Kocha Ernesto Valverde ana matumaini ya kuivusha Barcelona katika robo fainali ya mashindano hayo makubwa Ulaya.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Jumatano Machi 13 kwenye Uwanja wa Nou Camp, Hispania.