Messi anogesha mazoezi Argentina

Muktasari:

  • Argentina inatarajiwa kuvaana na Venezuela Ijumaa wiki hii kabla ya kuivaa Morocco Aprili 26 katika mechi za kirafiki. Messi aliibua mjadala katika fainali hizo baada ya kufunga bao moja tu katika mechi nne ambazo Argentina ilicheza. Bao hilo alifunga waliposhinda mabao 2-1 na Nigeria.

Buenos Aires, Argentina. Lionel Messi amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Argentina.

Messi hakufanya mazoezi na Argentina tangu alipotangaza kustaafu soka ya kimataifa.

Mshambuliaji huyo alitangaza kustaafu, baada ya Argentina kuboronga katika Fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Russia.

Nahodha huyo wa Barcelona, juzi alinogesha mazoezi ya Argentina akiwa na nyota wengine wanaocheza Ulaya.

Argentina inatarajiwa kuvaana na Venezuela Ijumaa wiki hii kabla ya kuivaa Morocco Aprili 26 katika mechi za kirafiki. Messi aliibua mjadala katika fainali hizo baada ya kufunga bao moja tu katika mechi nne ambazo Argentina ilicheza. Bao hilo alifunga waliposhinda mabao 2-1 na Nigeria.

Mchezaji huyo tayari amekosa mechi sita za kirafiki ambazo timu hiyo ilishinda nne na kutoka sare moja na kufungwa mchezo mmoja.

Kocha wa Argentina Lionel Scaloni alisema ataamua kama atampanga Messi katika mechi moja au mbili.