Messi mabao 40 kila mwaka kwa miaka 11 mfululizo

Muktasari:

Cristiano Ronaldo ambaye ndiye mpinzani mkubwa wa Messi na wamekuwa na mjadala usiokuwa na mwisho wa nani bora zaidi, amekuwa akifunga 40 tangu 2010, amepitwa kwa mwaka mmoja na nyota huyo wa Barcelona

Barcelona, Hispania. Lionel Messi amekuwa mchezaji wa kwanza duniani kufunga mabao 40 kila mwaka kwa miaka 11 mfululizo.

Messi alifunga mabao matatu ‘hat-trick’ mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Celta Vigo inamfanya kufikisha mabao 40 kwa mwaka huu kwa klabu nan chi yake.

Messi mwenye miaka 32, alifunga hat-trick kwa mabao mawili akifunga kwa mpira wa adhabu na penalti moja wakati Barcelona ikishinda 4-1 dhidi ya Celta Vigo kwenye Uwanja wa Nou Camp.

'Haiwezekani neno hilo halipo kwa Messi,' alisema kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde baada ya mchezo huo. 'Amefanya kila kitu. Tunatakiwa kujivunia kwa hilo. Ni kitu kinachotupa nafasi kubwa mbele ya wapinzani wetu kwa sababu yake.'

Mabao matatu ya Messi Jumamosi iliyopita yanamfanya kufikisha idadi ya mabao 40 kufunga kwa klabu na nchi yake ndani ya mwaka mmoja.

Cristiano Ronaldo ambaye ndiye mpinzani mkubwa wa Messi na wamekuwa na mjadala usiokuwa na mwisho wa nani bora zaidi, amekuwa akifunga 40 tangu 2010, amepitwa kwa mwaka mmoja na nyota huyo wa Barcelona.

BAO YA MESSI KWA MIAKA 11 ILIYOPITA

(Mabai aliyofunga kwa Barcelona na Argentina kila mwaka)

2009: 41

2010: 60

2011: 59

2012: 91

2013: 45

2014: 58

2015: 52

2016: 59

2017: 54

2018: 51

2019: 40