Kocha mpya Simba kuishudia Singida United

Thursday January 18 2018

 

By Thomas Ng’itu

Dar es Salaam. Hatimaye kocha mpya wa Simba, Mfaransa  Pierre Lechantre amesaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo kuanzia leo.

Kocha huyo anachukua nafasi ya Mcameroon Joseph Omog aliyetupiwa virago hivi karibuni baada ya mwenendo mbaya wa vinara hao wa Ligi Kuu Bara.

Mfaransa Lechantre leo ataishudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa atasaidia na kocha Masoud Djuma.

Kocha Lichantre keshawahi kufundisha klabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa ubingwa wa Africa 2000.

Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012.

Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi.

Advertisement