Michael Wambura aachana rasmi na soka

Muktasari:

  • Kumekuwa na sintofahamu kati ya Michael Wambura na mabosi wa TFF wakiongozwa na rais wao, Wallace Karia. Viongozi wa TFF wanadai Wambura si kiongozi wa Shirikisho hjilo lakini kiongozi huyo alipinga na kufungua kesi mahakamani.

Dar es Salaam. Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura ameamua kuachana na masuala ya mpira wa miguu.

Kwa mujibu wa taarifa kwa waandishi wa habari iliyotolewa na Wakili Emmanue Muga anayemsimamia kazi zake.

Katika taarifa hiyo,  Wambura ameamua pia kuondoa kesi iliyokuwa mahakamani. Kesi hiyo alifungua kwa ajili ya kukazia hukumu ya Mahakama juu ya uamuzi wa kufungiwa kwake na TFF hapo awali.

Hata hivyo katika taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, Wambura hajabainisha sababu hasa ya kuchukua uamuzi huo.

Taarifa za hivi karibuni zilidaiwa kuwa Wambura alishikiliwa na Takukuru kutoka na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha alipokuwa madarakani.