Mkenya aandika historia ya mbio za marathoni duniani

Saturday October 12 2019

 

Mwanariadha wa Kenya, Elliud Kipchoge amefanikiwa kumaliza mbio za marathoni kwa kutumia muda wa chini ya saa mbili.
Akiwa amevalia jezi nyeupe na kusaidiwa na wanariadha saba wa kumuongezea kasi (pace makers), Kipchoge, ambaye ni bingwa wa dunia na Olimpiki wa marathoni, alipita barabarani akiwa anashangiliwa. Alianzia darajani na kumalizia kwenye bustani ya Prater na kuweka rekodi ya dunia.
Kw miaka mingi, muda wa kumaliza mbio za marathoni umekuwa kuanzia saa mbili, lakini Kipchoge alipania kumaliza mbio hizo maalum kwa kutumia muda wa chini ya saa 1:59 na kuandika historia.
Huku mishale ya saa ikionyesha saa 1:59:40.2, bingwa huyo wa Olimpiki alivuka sehemu ya kumalizia na kuwa binadamu wa kwanza duniani kumaliza kilomita 42 chini ya saa mbili.

Advertisement