Mkude, Makame wakosekana mazoezini Taifa Stars

Muktasari:

  • Mkude alikuwepo katika kikosi cha Simba kilichocheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Tanzania Prisons, wakati Makame hakuichezea Yanga dhidi ya Ndanda.

Dar es Salaam. Kiungo wa Simba Jonas Mkude na Abdulaaziz Makame wa Yanga wamekosekana katika mazoezi ya leo asubuhi ya timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mkude alikuwepo katika kikosi cha klabu yake ya Simba kilichocheza mechi yake ya mwisho na Tanzania Prisons, lakini amekosekana katika mazoezi yanayoendelea uwanjani hapa.

Wachezaji wenzake wa Simba walioitwa Stars walikuwepo katika mazoezi hayo ni pamoja na Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Hassan Dilunga, Miraj Athuman na Mzamiru Yassin.

Naye kiungo wa Yanga, Makame aliyekosekana katika mchezo wa Ijumaa iliyopita dhidi ya Ndanda hakuwepo katikamazoeni Stars, huku Metacha Mnata na Kelvin Yondani wakishiriki katika maandalizi hayo.

Wachezaji wa Taifa Stars waliofanya mazoezi ya leo asubuhi ni pamoja na Metacha Mnata, Juma Kaseja, Dickson Job, Salum Kimenya, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Bakari Mwamnyeto, Danny Lyanga, Ditram Nchimbi, Hassan Dilunga, Shaban Chilunda, Hassan Kessy, Eliuter Mpepo, Miraj Athuman, Frank Domayo, Mzamiru Yassin, Idd Seleman, Salum Abubakary na Kelvin Yondani.