Mkutano Simba SC wachelewa kuanza wanachama 950 wajitokeza

Muktasari:

Saa 5:05 mkutano huo ulifunguliwa rasmi na kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda kwa kumtambulisha mgeni rasmi Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson.

Dar es Salaam Mkutano mkuu wa klabu ya Simba unaofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere umechelewa kuanza baada ya saa 3:40 asubuhi umeanza Saa 5:05 asubuhi.

Ratiba inaonyesha mkutano huo ulitakiwa kuanza saa 3:40 asubuhi na kumalizika saa 6:30 mchana, lakini mpaka kufika saa 4:45 asubuhi mkutano huo ulikuwa bado haujaanza na baadhi ya wanachama walikuwa wakilalamika mkutano huo kwenda nje ya muda.

Katika hatua nyingine licha ya mkutano huo kuchelewa kuanza viongozi wa Simba waliwasili ndani ya ukumbi saa 4:45 asubuhi huku baadhi ya mashabiki wakionekana kupiga makofi.

Kiongozi aliyepigiwa makofi mengi kuliko wote na wanachama akikuwa Ofisa mtendaji mkuu Senzo Mazingisa.

Jambo hilo huenda liliwafanya wanachama kuacha tena kulalamika kama ilivyokuwa hapo awali.

Saa 5:05 mkutano huo ulifunguliwa rasmi na kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda kwa kumtambulisha mgeni rasmi Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson.

Meneja mashindano Hamis Kissiwa, alitangaza mpaka muda huo wanachama walijitokeza walikuwa zaidi ya 950.

Kissiwa alisema wanachama wamejitokeza zaidi ya 950, mpaka sasa na kwa mujibu wa katiba yao mkutano unaruhusuwa kuanza.

"Mkutano wetu unaruhusiwa kuanza kutokana na idadi ya wanachama ambao wanefika na wanaendelea kujitokeza," alisema Kissiwa.

Mkutano mkuu wa klabu ya Simba unafanyika leo katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano Julias Nyerere hapa Posta mjini Dar es Salaam.