Moto wa Simba huko Afrika Kusini haupoi yaani!

Muktasari:

  • Kikosi cha Simba kimeweka kambi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika na mashindano mengine kwa ajili ya msimu ujao.

Dar es Salaam. Huko Afrika Kusini kikosi cha Simba unaambiwa hakipoi kabisa kutokana na shughuli wanayofanya.

Simba imeweka kambi katika mji wa Rustenburg nje kidogo ya mji kwa ajili maandalizi hayo tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita walipojificha Johannesburg.

Taarifa kutoka ndani ya kikosi hicho zinasema, timu inaendelea vizuri na mazoezi chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na Mbelgiji Patrick Aussems na wasaidizi wake, Dennis Kitambi na Mtunisia Adel Zrane.

"Mazoezi ya timu kwa ajili ya mashindano ya kimataifa na Ligi Kuu yanaendea vizuri na kila kitu kinakwenda vizuri,"ilisema taarifa hiyo.

Safari ya nje ya nchi kwa ajili ya maandalizi hayo kwa Simba si ya kwanza kwenye Afrika Kusini huku mwaka jana walikwenda Uturuki ambako walikaa kwa wiki mbili.

Wakati Simba ipo Afrika Kusini, watani wao wa jadi Yanga maandalizi yao wanayafanya mkoani Morogoro.