Mwakinyo aja na kauli mbiu ya do or die kumkabiri 'ndugu' wa Paquiao

Muktasari:

  • Mwakinyo ana rekodi ya kushinda mapambano 17 (15 kwa KO) amepigwa mara mbili moja kwa KO dhidi ya Mtanzania, Shaban Kaoneka.

Dar es Salaam. Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amekuja na kauli mbiu ya do or die (kufa ua kupona) katika pambano lake dhidi ya Arnel Tinampay litakalochezwa Novemba 29, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mwakinyo ambaye amekuja na kauli mbiu ya do or die (kufa na kupona) amesema anatambua ugumu wa pambano hilo ambalo litapigwa Novemba 29 kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mwakinyo atazichapa na Tinampay katika uzani wa super welter pambano la raundi 10 la uzani wa super welter.
Akizungumzia pambano hilo, Mwakinyo amesema anata liwe la heshima kwake kwani anamuona mpinzani wake kuwa bingwa zaidi yake.
"Mpinzani wangu ni bondia mgumu ana uzoefu na hana rekodi ya kupigwa Knock Out (KO), ni mgumu na anahitaji mbinu za ziada na mazoezi ili kumpiga," alisema Mwakinyo.
Alisema anajipanga kushinda pambano hilo kutokana na maandalizi ambayo anafanya kwenye gym yake iliyopo Makorola mjini Tanga ili kuendeleza rekodi yake kwenye ngumi ambapo sasa ni bondia namba 19 wa dunia kwenye uzani wa welter.
"Nitacheza kufa ua kupona kuhakikisha naendeleza rekodi yangu, natambua ugumu wa pambano hili na ubora wa mpinzani wangu ambaye ni bondia huyo ambaye ni namba mbili katika viwango vya ubora nchini Ufilipino kwenye uzani wa super welter," alisema.
Promota wa pambano hilo, Jay Msangi amesema Mwakinyo na Tinampay watasindikizwa na mapambano manne ya utangulizi ya mabondia kutoka nchini na nje ya nchi ambao watatajwa baadae.