Mwakinyo ndani orodha ya mabondia bora Duniani

Muktasari:

Mwakinyo ni bondia wa 19 wa dunia kwenye uzani wa super welter na namba moja Afrika na Tanzania katika uzani huo huku kwenye pound of pound amekamata nafasi ya 224.

Dar es Salaam. Wakati bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo akikamata nafasi ya 224 kwenye orodha ya mabondia bora wa dunia kwenye uzani tofauti (pound of pound), mabondia nguli, Manny Pacquiao na Andy Ruiz Jr wameshindwa kuingia 10 bora.

Mwakinyo mwenye nyota nne ni miongoni mwa mabondia wachache Afrika waliotamba katika rekodi hiyo huku Mmexico, Saul Alvarez akiwa ndiye kibara.

Mwakinyo ni bondia wa 19 wa dunia kwenye uzani wa super welter na namba moja Afrika na Tanzania katika uzani huo huku kwenye pound of pound amekamata nafasi ya 224.

Alvarez bondia wa uzani wa middle ameongoza akiwa na pointi 1637 huku Terence Crawford anayepigania uzani wa welter raia wa Marekani akikamata namba mbili akiwa na pointi 1489.

Mmarekani mwingine, Vasiliy Lomachenko anahitimisha tatu bora akiwa na pointi 1301 akipigania uzani wa light.

Bondia namba moja kwenye uzani wa welter Manny Pacquiao raia wa Ufilipino katika orodha hiyo amekuwa wa 10 nyuma ya bondia namba nne Gennady Golovkin wa Marekani (middle), Errol Spence Jr wa Marekani, (welter), Oleksandr Usyk wa Ukrane (cruiser),

Miguel Berchelt wa Mexico (super feather), Callum Smith wa Uingereza (super middle) na Leo Santa Cruz wa Marekani (feather).

Andy Ruiz ambaye pia ni bondia namba moja kwenye uzani wa juu katika orodha ya pound of pound amekamata namba tatu wakati mpinzani wake wa sasa, Anthony Joshua akiwa wa 23.