Mwamuzi Mabena kuzihukumu Simba na Yanga Taifa

Muktasari:

Mchezo huo wa watani wa jadi utazikutanisha Simba na Yanga vigogo wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku Simba wakiingia kwenye mchezo huo wakiwa na tofauti ya alama 22 ambapo Wekundu wa Msimbazi wapo nafasi ya nne huku Yanga wakiwa kileleni na pointi 58.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Mwamuzi Hance Mabena kuchezesha pambano la Simba na Yanga litakalofanyika kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo ilisema kwamba katika mchezo huo wa kesho Mabena ndiye atakuwa mwamuzi wa katikati, akisaidiwa na Mohamed Mkono pamoja na Kassimu Mpanga.

Pia taarifa hiyo ilieleza kwamba Elly Sasi ndiye atakuwa mwamuzi wa akiba.

Mchezo huo wa watani wa jadi utazikutanisha Simba na Yanga vigogo wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku Simba wakiingia kwenye mchezo huo wakiwa na tofauti ya alama 22 ambapo Wekundu wa Msimbazi wapo nafasi ya nne huku Yanga wakiwa kileleni na pointi 58.

Mechi hiyo huo umekuwa na msisimko nje ya uwanja kutokana na rekodi na historia timu hizo pinzani kutoka katikati ya jiji zinapokutana.